Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapokewa kwa shangwe ikiwazima Prisons

Mayele Arejea Tizi Yanga yapokewa kwa shangwe ikiwazima Prisons

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kutangulia uwanjani na uwenyeji wao wa mechi, lakini Tanzania Prisons imezidiwa shangwe na wapinzani wao Yanga wakati timu hizo zikiwasili Sokoine.

Timu hizo zinatarajia kukutana saa 9:30 alasiri katika mchezo wa ligi kuu ambao ndio wa mwisho msimu huu.

Baada ya mechi hiyo, Yanga atakabidhiwa kombe lao la ubingwa wa ligi hiyo ikiwa taji lao la 29 katika michuano hiyo mikubwa hapa nchini.

Prisons ndio walitangulia kufika uwanjani saa 7:44 ambapo hakukuwa na shamrashamra zaidi pengine kutokana na idadi ya mashabiki wao kuwa kiduchu na kwenda moja kwa moja chumba cha kubadilishia nguo.

Bingwa wa misimu miwili mfululizo, Yanga waliwasili saa 7:55 na kupokelewa kwa shangwe kuanzia geti kuu la kuingilia magari hadi chumba cha kubadilishia nguo walipopokelewa na mashabiki waliopo karibu na maeneo hayo.

Wachezaji Fiston Mayele, Kocha Mkuu Nassredin Nabi na Metacha Mnata ndio waliwapungia mikono mashabiki wao na kuamsha furaha uwanjani hapo.

Hata hivyo mastaa Benard Morrison, Khalid Aucho na Jesus Moloko baada ya kushuka kwenye gari walipitiliza jukwaa kuu kutokana na kuwa na kadi nyekundu na njano.

Chanzo: Mwanaspoti