Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapokea ofa ya mastaa watano wa kuwauza

Aziz Mokwena 2681708 Aziz Ki na Mokwena.

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema mpaka sasa klabu hiyo imeshapokea ofa za wachezaji watano kutakiwa na klabu mbalimbali za barani Afrika na Asia, ikiwemo uhitaji wa Aziz Ki.

Akizungumza nasi, Kamwe amesema Aziz Ki ofa zake zimekuwa zikijirudia; “Mtu kama Aziz ofa zake zinajirudiarudia tu, leo utakisikia kutoka South Afrika, kesho Morocco, kesho ofa Misri zinajirudia tu.”

Kamwe amesema baada ya ofa hizo kinachofuata ni kuzijadili kwenye uongozi kuona kama kuna uwezekano wa kuruhusiwa au kubaki nao, amesema wameshazungumza na baadhi ya wachezaji mambo yanaenda vizuri.

Pia Kamwe amegusia tetesi za Mzize kutakiwa na Azam FC, ambapo hakuthibitisha ila amesema alizungumza na Mzize na kumpa mawili matatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live