Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapinga Ngassa kufungiwa

93733 Yanga+pic Yanga yapinga Ngassa kufungiwa

Thu, 30 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imepinga adhabu iliyopewa na Kamati ya Saa 72 ambayo iliyowafungia wachezaji wake watatu na kutoa onyo kwa kocha Luc Eymael.

Bumbuli alisema kikao cha mwisho cha kamati ya saa 72, kiliamua kuwafungia wachezaji na kuitoza faini timu kwa makosa mbalimbali.

“Yanga hatukubaliani na adhabu hizo kwani kuna mambo mengi ya kisheria hayakufatwa mpaka kuamua kutoa hukumu hiyo ambayo awali tulipeleka malalamiko yetu kwa wasimamizi wa ligi lakini hatukupewa majibu.

“Tumeandika barua TFF, CAF, Fifa, Takukuru na mamlaka nyingine husika kulalamika juu ya hilo,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Mnguto alitangaza kuwafungia mechi tatu na faini ya Sh 500,000 kwa wachezaji wa Yanga, Ramadhani Kabwili, Mrisho Ngassa, Cleofas Sospeter baada ya kugoma kutoka uwanjani katika pambano la ligi dhidi ya Mbeya City.

Yanga ilitozwa faini Sh 500,000 baada ya kushindwa kuwasilisha kikosi katika mechi ya ligi dhidi ya Prisons.

Pia Soma

Advertisement
Pia Yanga katika mchezo dhidi ya Simba ilitozwa faini nyingine ya Sh 200,000 kwa wachezaji na benchi la ufundi kushindwa kutumia vyumba rasmi vya kuvalia nguo wachezaji ambavyo ni maalumu kwa ajili hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz