Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapigwa, Simba yalazimishwa sare

IMG 4352.jpeg Yanga yapigwa, Simba yalazimishwa sare

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo, Simba na Yanga wameanza kwa kusuasua Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 katika mechi zao za leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Wakati Simba imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar katika mchezo wa Kundi D, Yanga imechapwa 1-0 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Kundi B.

Mechi nyingine za leo, Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu katika mchezo wa Kundi D, wakati Tanzania Prisons imeitandika Polisi Tanzania 4-2 katika mchezo wa Kundi B mechi zote zikichezwa hapo hapo Chamazi Alhamisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live