Thu, 28 Sep 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kosa la kuwakilishwa na kocha mkuu (Miguel Angel Gamondi) pekee kwenye mkutano wa Wanahabari kuelekea mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliomalizika Kwa Yanga kuibuka na ushindi wa 5-0.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 17:56 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, kocha huyo alipaswa kuambatana na nahodha wa timu au mchezaji mwenye ushawishi kwenye timu.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: