Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapewa mbinu za ubingwa

Yangapic Data Kikosi cha Yanga

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Staa wa zamani wa Yanga na mchezaji msomi wa klabu hiyo, Ally Mayay amelisisitiza benchi la ufundi la timu hiyo kutumia mbinu mbadala kuwarudisha wachezaji mchezoni. Kocha Mkuu Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedrick Kaze wako kwenye presha kubwa kutokana na kasi ya Simba ambayo inazidi kupunguza pointi kila kukicha.

Yanga imecheza mechi tatu mfululizo bila kupata bao licha ya kutengeneza nafasi nyingi ndani ya mechi ilizocheza huku mshambuliaji wao Fiston Mayele mwenye mabao 12 akikosa penalti kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons.

Akizungumza nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay alisema ili Yanga ipate matokeo mazuri mechi ijayo morali ya wachezaji wake inatakiwa kuwa juu kama ilivyokuwa michezo ya mzunguko wa kwanza.

Yanga leo inacheza na Dodoma Jiji mechi ya Ligi Kuu Bara raundi ya 24, mechi hiyo itapigwa saa 10:00 Jioni kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

“Yanga wanaonekana kuwa bora ndani ya dakika 90 kwani kama pasi wanapiga na nafasi za mabao zinatengenezwa lakini bado kuna kitu muhimu wanatakiwa kukifanyia kazi ambacho ni kujenga saikolojia ya wachezaji wao ili wafanye vizuri na kuwa katika fomu waliyokuwa nayo mzunguko wa kwanza,” alisema.

“Kutokana na msimamo ulivyo kwa sasa Yanga inatakiwa kushusha presha kwani kufanya hivyo kutawafanya wachezaji wake kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ndani mchezo.

“Hii inasababishwa na mmoja wao kuzikosa mechi nyingi ambazo kama angekuwa anacheza basi huenda angeboresha zaidi kasi yake lakini tofauti na hapo lazima mmoja wao awe na kasi tofauti na mwenzake.” alisema. Katika msimamo Yanga ipo kileleni na pointi 57 baada ya kucheza michezo 23. Simba ina pointi 49.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz