Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapewa Ubalozi wa Kupinga Ukatili kwa watoto

Yanga Balozi Yanga yapewa Ubalozi wa Kupinga Ukatili kwa watoto

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametangaza kuwa klabu ya Yanga ni mabalozi wapya wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto.

Akizungumza hii leo Aprili 14 katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Waziri Gwajima amesema;

"Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Young Africans SC kuwa Mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto" Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Nae Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akipokea Ubalozi huo kwa niaba ya Klabu amesema;

"Naungana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika kampeni ya kupinga mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto"

"Napenda kutoa rai kwa vilabu vya Simba SC, Azam FC, KMC na vingine vyote kuunga mkono kampeni hii, kampeni hii siyo mashindano ya kibiashara sote kwa pamoja tuungane na Mhe. Waziri kutokomeza changamoto hizi kubwa na kuilinda jamii yetu"

"Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Klabu zetu ndio waathirika wakubwa wa hii vita dhidi ya ukatili wa kina mama na watoto, tusipowalinda kuna siku tutacheza mpira bila mashabiki Uwanjani"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live