Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaongeza mashushu Sudan

Yanga Vs Al Hilal Yanga yaongeza mashushu Sudan

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imedhamiria kwenda kusaka matokeo ya ushindi Sudan ili kuhakikisha inatinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Ili kuepuka hujuma za aina yoyote kutoka kwa wenyeji wao, tayari maafisa wa Yanga wametua Sudan kuweka mambo sawa.

Uongozi wa Yanga unahakikisha kikosi kinakuwa katika mazingira bora kitakapokuwa Sudan kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumapili Oktoba 16.

Pamoja na kuwa Yanga iliwapa Al Hilal ukarimu wa hali ya juu walipokuja nchini, hakuna uhakika kama wenyeji wao nao watalipa ukarimu.

Tayari kuna taarifa kuwa Al Hilal wamewagomea Azam TV kuonyesha mchezo huo 'mbashara' hivyo kuna uwezekano mchezo hautaonyeshwa na televisheni yoyote.

Al Hilal walifanya hivyo kwenye mchezo wao dhidi ya St George ambao walishinda kwa bao 1-0, kupitia mkwaju wa penati ya Makabi Lilepo.

Silaha kubwa ya Yanga kuelekea mchezo huo ni ubora wa kikosi na mbinu za Kocha Nasreddine Nabi. Yanga inatarajiwa kutoa nafasi kwa mashabiki ambao watapenda kuiunga mkono huko Sudan.

Huenda Wananchi wakapaa na 'dege' la ATCL siku chache kabla ya mchezo na kurejea baada ya mchezo huo ili kuwahi maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live