Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaomboleza vifo Hanang kimataifa

Yanga Hanang Yanga yaomboleza vifo Hanang kimataifa

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga Iko uwanjani muda huu ikicheza mechi ya ugenini dhidi ya Medeama ya Ghana lakini ikautumia mchezo huo kuomboleza vifo vya janga la mafuriko yaliyotokea Hanang Mkoa wa Manyara.

Katika mchezo ambao unaendelea Sasa wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaopigwa Uwanja wa Baba Yara wachezaji wa Yanga wamefunga vitambaa vyeusi katika mikono yao ya kushoto.

Hata hivyo uamuzi huo wa Yanga umepata baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo mabingwa hao wa Tanzania waliwasilisha maombi ya kutumia mchezo kuomboleza vifo hivyo.

Mapema Yanga kupitia Rais wao Hersi Said wakitangulia kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko hayo wenye thamani ya sh 40 milioni.

Mpaka Leo Desemba 8 mchana serikali imetangaza idadi mpya ya vifo kufikia watu 80 vilivyotokana na mvua kubwa iliyonyesha alfajiri ya Desemba 3 na kuporomosha matope,mawe na magogo kutoka Mlima Hanang, wilayani Hanang Mkoa wa Manyara.

Katika vifo hivyo watu wazima ni 48 wakiwemo wanaume 19, wanawake 29 huku watoto wakiwa 32 ambapo wakiume ni 15 na wa kike 17

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: