Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaomboleza kifo cha Ally Sonso

Yanga Yaomboleza Yanga yaomboleza kifo cha Ally Sonso

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imepokea kwa masikitiko Makubwa kifo cha aliekuwa beki wake Ally Mtoni Sonso kilichotokea Jioni ya Februari 11 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa yake klabu ya Yanga imeandika

"Tunasikitika kutangaza kifo cha Sentahafu wetu wa zamani Ally Mtoni Sonso kilichotokea leo kwenye Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa zaidi juu ya taratibu za mazishi tutaendelea kuwaarifu.

Sonso anakumbukwa kwa mengi ikiwemo ujasiri wake ndani ya Uwanja, nidhamu pamoja na kujitolea kuipigania Jezi ya team yetu.

Tunamuombea kwa Mungu aipokee roho ya mpendwa wetu Ally na pia tunatoa pole kwa wafiwa wote, hususan familia yake".

Inna lillah Wainna Ilaihi Raajiuun

Chanzo: www.tanzaniaweb.live