Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yanasa mwingine Congo DR

Basiala Pic Yanga yanasa mwingine Congo DR

Tue, 14 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati ikitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya 30 baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 3-1, kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro, Klabu ya Yanga inahusishwa kutaka kuwasajili nyota wawili, kiungo mshambuliaji Agee Basiala kutoka Klabu ya AS Maniema ya DR Congo na kipa wa Tanzania Prisons, Yona Amos kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano.

Imeelezwa kuwa tayari uongozi wa timu hiyo upo kwenye mazungumzo na wachezaji hao, na kwamba kwa upande wa Basiala mwenye uwezo wa kucheza namba nane na 10 pia akiweza kutokea pembeni, alifanya mazungumzo na Rais wa Yanga, Hersi Said, alipokuwa nchini DR Congo wiki iliyopita.

Pia Yanga, ipo katika harakati za kuhitaji huduma ya kipa Amos, anayewindwa na Wanajangwani hao  kuchukua nafasi ya, Metacha Mnata, ambaye tetesi zinaeleza atapewa mkono wa kwa heri mwishoni mwa msimu.

Taarifa za uhakika zilizolifikia Nipashe Digital, kutoka ndani ya Yanga, Hersi amefanya mazungumzo na kipa huyo ili kuiongezea nguvu timu yao sambamba na kiungo wa kati Yusuph Kagoma aliyekuwa Singida Fountain Gate FC. 

"Mkakati mwingine wa mpango wa klabu unahusisha kipa wa Tanzania Prisons, Yona Amos ni chaguo la kwanza kwa sasa, Yanga inalenga kupata huduma yake ili kuimarisha safu yao ya ulinzi na kuzidi kuimarika kama kikosi kikali katika soka la Tanzania," amesema mtoa habari huyo ndani ya Yanga.

Ameongeza kuwa mazungumzo na kipa huyo bado yanaendelea, na kwamba Yanga imeendelea kujikita katika kudumisha hadhi yake ya kutawala soka la Tanzania, macho yakiwa yanalenga kuendelea kufanikiwa ndani na kimataifa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema mambo yanaenda vizuri na kila kitu kinasimamiwa ipasavyo na rais wa klabu hiyo, ambapo matumaini makubwa msimu ujao ni kuona Wananchi wakifurahi.

Katika hatua nyingine kikosi cha Yanga leo kinashuka dimbani katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Manungu Complex uliopo Tuliani,  Morogoro.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema maandalizi yaneenda vizuri na wanaiheshimu Mtibwa Sugar kwa sababu ipo nyumbani na wapo nafasi ya chini, hivyo itakuwa ikitaka kujinasua kwa kupata matokeo chanya. 

"Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu wapinzani wanaingia na presha kubwa ya kutaka matokeo chanya, wachezaji wako tayari kwa mchezo huo kwa kupambana kusaka alama tatu," amesema kocha huyo.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wanafahamu ubora wa Yanga na wamejipanga kutafuta pointi muhimu katika mchezo wa leo ili kujinusuru na kushuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live