Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yamtambulisha kiungo wa kazi, Aziz Andambwile

Andambwileee M0n.jpeg Yanga yamtambulisha kiungo wa kazi, Aziz Andambwile

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Aziz Andambwile (24) amejiunga na Yanga akitokea Singida Fountain Gates (Fountain Gate) kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Andambwile ambaye ni kiungo mkabaji, anaenda kuongeza nguvu eneo ambalo linachezwa na Khalid Aucho na Jonas Mkude pale Yanga.

"Kiungo wa kazi Aziz Andambwile amejiunga na Young Africans SC akitokea Singida Fountain Gates.

Usajili wa kiungo huyo ni sehemu ya kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa 2024-2025.

Andambwile ni kiungo mkabaji, anakuja Young Africans SC kuongeza nguvu eneo hilo ambalo linachezwa na Khalid Aucho na Jonas Mkude.

Kiungo huyo anasifika kwa kucheza soka la utulivu na kupiga pasi za uhakika kwa wenzake anapokuwa uwanjani.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakiitumikia Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Andambwile anakuwa mchezaji wa tano mpya kutambulishwa ndani ya Young Africans SC kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa baada ya Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Khomeiny Aboubakar,"
imesema taarifa ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live