Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yampa mkono wa kwaheri Mukoko Tonombe

Tonombe Aagwa Mukoko Tonombe akiwa na Injinia Hersi, wakati akisajiliwa kujiunga na Yanga

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu Yanga imetangaza kuachana rasmi na aliyekuwa kiungo mkabaji wa timu hiyo Tonombe Mukoko baada ya kuitumikia kwa takribani misimu miwili.

Yanga imeachana na mchezaji huyo kwa kile ambacho kinaelezwa kuwa kumefanyika mabadilishano ya wachezaji, ambapo Timu ya Wananchi imemchukua Chiko Ushindi wakati Tonombe akielekea TP Mazembe.

Taarifa ya Yanga jioni hii imemshukuru Mukoko kwa mchango wake kama Nahodha Msaidizi kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu tangu awasili kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa.

Mukoko anakwenda Mazembe wiki moja baada ya Yanga kumsajili Mkongo mwingine, winga Chico Ushindi kutoka klabu hiyo ya Lubumbashi.

Tazama hapa chini kuona taarifa ya Yanga, ikimuaga kiungo huyo;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live