Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yampa 'Thank you' Metacha Mnata

Metacha Gh Metacha Mnata

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba mbili wa Young Africans Sports Club, Metacha Boniphace Mnata hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao wa 2024-2025.

Klabu ya Yanga imempa mkono wa kwa heri Metacha baada ya kuitumikia timu kwa msimu mmoja na nusu.

Kipa huyo alijiunga na kikosi hicho Januari 2023 akitokea Singida Big Stars ambapo wamekuwa naye kwa vipindi viwili tofauti.

Mara ya kwanza Metacha alijiunga na Young Africans Agosti 2019 akitokea Mbao FC kisha akaondoka 2021 kabla ya kurejea kwa Wananchi mwaka 2023.

Metacha anatajwa kuwa huenda akatua katika Klabu ya Singinda Black Stars na atatambulishwa siku yeyote kuanzia sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live