Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yalazimishwa sare na JKU Avic Town

Yanga Sare Yanga yalazimishwa sare na JKU Avic Town

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana jioni Yanga SC ilicheza mechi ya kirafiki na kutoka sare ya bila kufungana na JKU ya Zanzibar Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima kwa jana pekee kwa Yanga baada ya asubuhi kuibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Friends Rangers.

Kwa ujumla Yanga imecheza mechi nne za kujiandaa na msimu chini ya kocha mpya, Muargentina Miguel Angel Gamondi, nyingine mbili ikishinda 1-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na 10-0 dhidi ya Magereza ya Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: