Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yalaani shabiki kupigwa Uwanja wa Mkapa

Shabiki Apigwa Yanga yalaani shabiki kupigwa Uwanja wa Mkapa

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kupitia mitandao ya kijamii kumesambaa video ikionyesha shabiki aliyevaa jezi ya Yanga akishambuliwa na mashabiki waliovalia jezi za Simba katika Uwanja wa Mkapa.

Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick ameandika kupitia akaunti yake kuwa kesho Oktoba 30 klabu hiyo itawasilisha malalamiko yake na kuomba hatua kali zichukuliwe.

“Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisaa, hakuna sababu ya msingi ya kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni watani wa jadi sio maadui,”

Ameongeza; “Naiomba Bodi ya Ligi Kuu, Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jeshi la Polisi wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe,”

Chanzo: Mwanaspoti