Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yakwaa kisiki Kagame Cup

Yanga Nje Pic Data Heka heka za wachezaji wa timu ya yanga na Express Uwanjani

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Soka ya Yanga imetupwa nje katika michuano ya vilabu afrika Mashariki na kati maarufu kama Cecafa Kagame Cup.

Yanga imeyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo kitakatifu cha mabao 3-1 kutoka kwa timu ya Express FC ya nchini Uganda,na kuifanya Yanga kutoshinda mchezo wowote baada ya kutoa sare michezo miwili na kupoteza mmoja katika Kundi A.

Katika ushindi huo mnono ,magoli ya Express FC yamefungwa na Godfrey 14',Muzamiru 35' na kambale wakati bao pekee la Yanga lilifungwa Paul 71' na kuipa nafasi timu ya Express kutinga hatua inayofuata ya nusu finali ambapo itakutana na timu ya KMKM.

Katika mchezo mwingine wa Kundi A,Nyasa Fc imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Atlabara FC na kujihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live