Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yakusanya Sh1 bilioni usajili wanachama

Yanga Bilioni Yanga yakusanya Sh1 bilioni usajili wanachama

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Yanga imeweka wazi kwamba mchakato wa usajili wa wanachama umeiingizia klabu hiyo kiasi cha Sh1 bilioni kupitia ada za uanachama.

Mohammed Kirra Mtendaji Mkuu wa Kilinet amesema katika kipindi cha miezi sita ambayo wamekuwa wakisajili wanachama wa klabu hiyo wamefanikiwa kukusanya kiasi cha sh 1.07 bilioni.

Kirra amesema kiasi hicho kimetokana na usajili wa wanachama jumla 34,650 ambao kila mmoja amekuwa akilipa ada ya sh 29,000.

"Tumekuwa tukisafiri mikoa mbalimbali na takwimu zinaonyesha katika mkoa ambao umeongoza kwa usajili wa idadi kubwa ya wanachama ni Dar es Salaam ambao tulisajili wanachama 12124," amesema Kirra.

"Kwa upande wa Kanda takwimu zetu zinaonyesha kwamba Pwani ndio imeongoza kwa kutupatia wanachama 15,804.

Aidha Kirra ameongeza kuwa baada ya mafanikio hayo ya eneo la usajili wa wanachama sasa wataingia katika sura nyingine ya usajili wa mashabiki ambao watakuwa wakilipa kiasi cha sh 17,000 kwa ada ya mwaka.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz