Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yakomba Tsh bilioni 4.5

Yangas Aziz Kiii Yanga yakomba Tsh bilioni 4.5

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni fedha ndefu! Hivyo ndiyo unaweza kusema baada ya Yanga kufanikiwa kutwaa ubingwa wa FA ambao unawafanya wakusanye kitita kikubwa cha fedha msimu huu baada ya awali kuchukua kombe la Ligi Kuu.

Yanga msimu huu, imeweka rekodi nzito ikikusanya jumla ya Tsh bilioni 4.5 kutoka kwa wadhamini, fedha zilizotokana na makombe mawili iliyochukua huku ikifika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hiki ni kiwango kikubwa cha fedha kwa timu ya Ligi Kuu Tanzania kuwahi kuzoa baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi na Kombe la FA, tofauti na misimu kadhaa iliyopita.

Mchanganuo wa fedha ilizopata Yanga;

Azam TV - Bingwa wa Ligi Kuu - Tsh milioni 500

NBC - Bingwa wa Ligi Kuu - Tsh milioni 100

CRDB - Bingwa Kombe la Shirikisho - Tsh milioni 200

SportPesa -Bingwa Ligi - Tsh milioni 150

SportPesa - Bingwa Kombe la Shirikisho la CRDB -Tsh milioni 112

Azam TV - Bingwa Kombe la Shirikisho la CRDB - Tsh bilioni 1.1

Robo Fainali CAFCL - Tsh bilioni 2.3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live