Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yajipigia Kurugenzi FC nane mtungi (8-0)

Yanga Hii Balaa Yanga yajipigia Kurugenzi FC nane mtungi (8-0)

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa mtetezi wa wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Young Africans 'Yanga'wameshusha kipigo kikubwa kwa Kurugenzi FC kwenye mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya kombe hilo.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Dimba la Mkapa jioni ya lwoz Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 8-0 sawa na ushindi ambao walipata wapinzani wao Simba dhidi ya Eagle Fc jana.

Yanga walipumzisha mastaa wao karibu wote wa kikosi cha kwanza wengi na kuwapa nafasi wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi za kuanza katika kikosi cha mwalimu Nasreddine Nabi.

Straika kinda na mzawa ndani ya Yanga, Clement Mzize amefanikiwa kuondoka na mpira baada ya kufunga bao 4 peke yake katika mchezo huo.

Wafungaji; ⚽⚽⚽⚽ Clement Mzize dakika ya 1' 8' 42' na 45+4'

⚽ Jefta John (goli la kujifunga) dakika ya 5'

⚽ David Bryson dakika ya 77'

⚽⚽ Yusuf Athumani dakika ya 78' na 85'

Matokeo ys mechi za leo

FT Yanga SC 8-0 Kurugenzi FC

FT Tz Prisons 7-1Misitu FC

FT Siginda Big Stars 2-0 Lipuli FC

FT KMC 6-1 Tunduru Korosho FC

FT Kigoma Kwanza 0-1 Buhaya FC

FT Namungo FC 2-2 Kitayosce FC (Penalty 3-1)

FT Polisi TZ 3-0 Nyika FC

FT Mtibwa Sugar 2-0 TRA FC

VIPIGO VIKUBWA ASFC RAUNDI YA PILI

1. Azam Fc 9-0 Malimao

2. Ihefu Sc 9-0 Mtama Boys

3. Simba Sc 8-0 Eagle Fc

4. Yanga 8-0 Kurugenzi Fc

6. Tz Prisons 7-1 Misitu Fc

7. KMC 6-1 Tunduru Korosho

8. Mbeya city 5-1 Stand Fc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live