Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yajipanga kuwakabili Singida Big Stars

Tanga Mapinduzi Kks Yanga yajipanga kuwakabili Singida Big Stars

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema mchezo wa mwisho wa makundi Kombe la Mapinduzi dhidi ya Singida Big Stars Janauri 6 utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha timu hiyo ya Singida.

Kwa mujibu wa tovuti ya Yanga Kaze amesema lakini kama vijana wake watakuwa makini na kucheza kwa kujiamini basi bila shaka nafasi ya kufanya vizuri bado ipo.

“Tuliwaona Singida kwenye mechi ya kwanza, ni timu nzuri na wamekuja kwenye mashindano haya na kikosi chao kamili,” amesema Kaze.

Mchezo huo ndio utakaoamua nani anafuzu kutoka kwenye kundi baada ya timu hizo mbili kulingana pointi mpaka sasa.

“Naamini utakuwa mchezo mzuri sana kwani wachezaji wameonyesha kujiamini na kuwa tayari na mchezo huo. Ni imani yangu mazoezi ya leo yatatupa maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo,” amesema Kaze.

Mchezo wa kwanza Singida Big Stars walishinda bao 2-0 dhidi ya KMKM huku Yanga ikiichapa KMKM BAO 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live