Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yajibu madai ya kuwa Chama lazima aanze kikosi cha kwanza

Clatous X Chamaaaaaa Yanga yajibu madai ya kuwa Chama lazima aanze kikosi cha kwanza

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imejibu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa kiungo mshambuliaji Clatous Chama hana furaha ndani ya kikosi hicho kutokana na kocha Miguel Gamondi kutomwanzisha kwenye kikosi cha kwanza tangu asajiliwe kutoka Simba.

Taarifa hizo zimekuwa zikidai kuwa, kwenye mkataba wake na Yanga, Mwamba wa Lusaka anatakiwa kuanza kikosi cha kwanza iwapo atakuwa fit na hana majeraha wala tatizo lolote.

Msemaji wa Klabu ya yanga, Ally Kamwe amesema; "Hakuna kipengele kinachotaka Chama aanze, na sio Chama tu , mchezaji yoyote wa yanga hakuna kipengele kinachotaka aanze Kikosi cha kwanza. Hizo ni propaganda watu wameanzisha kwa sababu wanatafuta faraja," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: