Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaja na Black Card, unapata huduma zote za kifedha

Iyanga 70x650 Yanga yaja na Black Card, unapata huduma zote za kifedha

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga na Bank ya NMB, leo wamezindua kadi maalum za Wanachama wa Yanga ijulikanayo kama Black Card ambayo imeunganishwa na akaunti na huduma zote za kifedha za Benki ya NMB.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wa taasisi hizo mbili kubwa hapa nchini.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuzindua kadi hiyo, Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said, alisema:

“Nawapongeza sana NMB kwa hili ambalo wamefanya leo. Katika kukuza usajili wa Wanachama nadhani mwendelezo huu unaleta picha ya tofauti kabisa kwenye mapinduzi, sio tu ya Young Africans SC bali kwa soka la AFRIKA. Black Card ni kadi ya kiwango cha juu kabisa katika mapinduzi ya soka Tanzania.

“Tumefungua mlango maalumu kabisa kwa wanachama wetu kupata huduma za ziada. Hivyo Yanga tumekaa na NMB na kufungua majadiliano kuhakikisha wanapata huduma imara na madhubuti. Na kadi hizi zinatolewa katika matawi yote ya NMB.

“Thamani ya Black Card ni Tsh 1,000,000. Tumefanya utafiti maalumu kuhakikisha kadi hii inampa mwanachama wetu thamani na huduma bora na za kisasa kuhakikisha tunamthaminisha na kumuongezea faida ya kuwa mwananchama wetu.

“Mwanachama atapata tiketi 10 za VIP msimu mzima (thamani ya tiketi ya VIP 30,000). Mwanachama atapata jezi seti sita za msimu mpaka jezi za watoto (thamani ya jezi 50,000). Kadi hii itamwezesha kupata punguzo la huduma ya afya katika Hospitali ya Aga Khan kuanzia 10%+. Mwanachama mwenye “Black Card” atapewa kipaumbele cha kupata jezi mpya za msimu.”

Kwa upande wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB, Filbert Mponzi, alisema: “Mwaka jana mwezi Julai tulisaini makubaliano ya kushirikiana na Yanga SC kujisajili matawi yote ya NMB. Leo tumekuja tena kuzindua black card (World Debit MasterCard) kwa ajili ya wateja maalumu ambao ni Wanachama wa Klabu ya Young Africans na NMB.

“Miongoni mwa faida ya Black Card utapata fursa ya kuingia VIP LOUNGE katika kiwanja chochote cha ndege duniani. Black Card ina bima endapo utapoteza mzigo wako safarini unalipwa dola 3000.

“Endapo mzigo wako pia utachelewa utalipwa dola 300. Ikitokea unasafiri kwa ndege ndani ya nchi au nje ya nchi ndege ikaahirisha safari unalipwa mpaka dola 7500. Muhimu ni kuhakikisha unanunua tiketi ya ndege ili uweze kunufaika na BIMA ya namna hii.

“Ukiwa na Black Card, unaweza kupata mkopo mpaka 500,000 bila kufuata utaratibu wowote unaingia tu kwenye menyu yako au APP yako ya NMB unajipekulia mkopo. Vilevile ukienda baadhi ya sehemu za kupata chakula ukalipia na Black Card unapata punguzo mpaka 15%.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live