By Thobias SebastianMore by this AuthorBy Olipa AssaMore by this Author FURAHA imerejea tena Jangwani, baada ya nyota wao kutoka Angola, Carlinhos kufunga bao pekee lililowazamisha Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Katika kipindi cha kwanza mchezo huo ulimalizika bila mabao licha ya kosa kosa nyingi kwenye muilango ya timu zote.
Katika mechi hiyo Yanga walianza kwa kasi ya kupeleka mashambulizi aina tofauti katika lango la Mtibwa na yote yalipotea kwa kuokolewa na mengine kutoka nje.
Yanga ndani ya dakika 10, za mwanzo walifanya mashambulizi ya mara kwa mara kupitia kwa winga wake wa kulia, Ditram Nchimbi ambaye kuna wakati alifanikiwa kumpita beki wa kushoto wa Mtibwa, Issa Rashid na kuleta hatari ila muda mwingine alishindwa.