Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaiwinda KMC

Musonda Okrah Guede Kikosi cha Yanga wakifanya mazoezi.

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Yanga, jana Jumatano kimefanya mazoezi ya mwisho Avic Town, kabla ya leo kuanza safari kuelekea Morogoro kuikabili KMC.

Young Africans SC ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikikusanya pointi 40, Jumamosi ya wiki hii Februari 17, 2024 itakuwa ugenini kupambana na KMC.

Mchezo huo wa kwanza katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo, unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mpaka sasa, wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo, huku tukimkosa kipa Metacha Mnata pekee anayeitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live