Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaishushia mvua ya magoli Vital'O, Chama kazaliwa upya Jangwani

Yanga  1536x1129.jpeg Yanga yaishushia kipigo kizito Vital'O, Chama kazaliwa upya Jangwani

Sat, 24 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (Yanga SC) ya jijini Dar es Salaam wametinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Ni baada ya ushindi wa jumla ya mabao 10-0 dhidi ya Vital'O FC kutoka nchini Burundi katika mchezo wa hatua ya awali.

Full - Yanga 6 - 0 Vital'O

⚽️ Pacome Zouzoua (Pen) — dakika 13'

⚽️ Clement Mzize ›› Assist ya Chama — dakika 48'

⚽️ Clatous Chama — bao dakika ya 50'

⚽️ Prince Dube ›› Assist ya Chama — 71'

⚽️ Aziz Ki ›› Assist ya Chama — dakika ya 79'

⚽ Mudathir Yahya ›› Assist ya Chama dakika ya 84.

Aggregate - 10-0.

Yanga SC na Vital’O FC zimeumana katika mchezo wa marudiano Agosti 24,2024 katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar Es Salaam.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzou ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao hayo baada ya dakika ya 14' kipindi cha kwanza kuzifumania nyavu za Vital’O.

Naye Clement Mzize alitupia bao la pili katika dakika ya 49 ya kipindi cha pili cha mtanange huo, huku dakika ya 51 kiungo, Clatous Chota Chama akipachika bao la tatu.

Prince Dube dakika ya 72 alichomeka msumari mwingine, na Stephanie Aziz Ki akagonga mwingine dakika ya 78.

Huku, Vital’O wakiendelea kutafakati kuhusu kipi kimewasibu, dakika ya 86 Mudathir Yahaya Abbas alipachika bao la sita.

Hadi dakika 90 zinatamatika ubao ulikuwa unasoma Young Africans Sports Club mabao 6 huku Vital’O ubao ukisoma 0.

Yanga imeshinda mechi zake kwa jumla ya mabao 10-0 baada ya kuizaba Vital’O mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza Agosti 17,2024 katika dimba hilo.

Aidha, mchezo ujao itamenyana na Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE SA) kwenye raundi ya kwanza kutafuta tiketi ya hatua ya makundi ya CAFCL 2024/25.

Ni baada ya CBE SA kutoka sare ya bao 1-1 na Villa SC, na kushinda kwa jumla ya mabao 3-2.

Waethiopia hao waliwazaba Waganda mabao 2-1 wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Sazza Grounds huko nchini Uganda wiki iliyopita katika mechi ya kwanza.

Hata hivyo, baada ya mtanange huo,Msemaji wa Vital’O FC, Arsene Bucuti amekiri kuwa, Yanga SC ni timu bora zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Pia, amesema kucheza na Yanga ni kama kuacha kusoma shule ya msingi na kwenda shule ya sekondari huku akiwashukuru Watanzania kwa mapokezi mazuri tangu walipoingia hapa nchini.

Ushindi huo wa mabao 10 umeiwezesha Young Africans Sports Club kuchukua shilingi milioni 50 za hamasa kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan

Clatous Chama ameandika rekodi kuwa mchezaji wa kwanza CAF Champions League kutoa assists (4) katika mechi ya leo na kufunga bao 1. Clatous Chama amehusika kwenye magoli (7) katika mechi (3) za mwisho.

◉ vs Azam FC - Assist 1

◉ vs Vital'O - Bao 1

◉ vs Vital'O - Bao 1 na Assists 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live