Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaishushia kipigo kizito Namungo, yajikita kileleni

Yanga 0006 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao.

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dozi ya Young Africans SC katika Ligi Kuu ya NBC, imeendelea ambapo leo Ijumaa, Machi 8, 2024 ilikuwa zamu ya Namungo FC.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi, Young Africans SC imeibuka na ushindi wa magoli 3-1 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Magoli matatu ya Yanga yamefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 54, Clement Mzize (dk 57) na Stephane Aziz Ki (dk 62).

Aziz Ki goli lake la leo linamfanya kufikisha magoli 11, huku Mudathir akifikisha 7 ambapo msimu huu Mudathir ameifunga Namungo nyumbani na ugenini.

Young Africans SC kwa ushindi huo imefikisha pointi 46 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza mechi 17, ikiwa na mechi tatu mkononi dhidi ya Azam FC waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 43.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: