Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaishitaki CAF kwa FIFA

Semajiiii Msemaji wa Yanga, Haji Manara

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwakosa wachezaji wao watatu kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa Habari, Msemaji wa Yanga Haji Manara, amesema kukosekana kwa wachezaji hao hakuna makosa yoyote yaliyosababishwa na klabu yao ambapo matatizo hayo yamesababishwa na makosa ya klabu walizotokea wachezaji hao kwa kushindwa kuachia hati za uhamisho (ITC)kwa wakati.

"Yanga ilifanya kila kitu kwa wakati katika kuomba hati za uhamisho mchezaji kama Khalid Aucho alikuwa na mgogoro na klabu yake hawakumlipa mishahara yake na Fifa wakamvunjia mkataba na kuwa mchezaji huru," amesema Manara.

"Djuma Shaban naye tuliomba vitu vyote kwa wakati lakini klabu yake wakatoa ITC siku moja baada ya dirisha kufungwa hapo Yanga inakosa gani.

Aidha Manara ameongeza kwamba kutokana na changamoto hizo tayari uongozi wa klabu yao umeshaandikia barua FIFA kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF ) kuwaomba Fifa kuingilia kati suala hilo la Yanga kuzuiliwa wachezaji wake hali ya kuwa wao kama klabu walifanya kila kitu ndani ya muda.

"Tunaamini wenzetu wa Fifa watatupa majibu mazuri lakini hata hivyo mpaka kufikia siku ya jumapili kama hawajatupa majibu Yanga imejiandaa vizuri na kikosi ni kipana wapo wachezaji hata wakikosekana hao wapo ambao wataziba nafasi zao."

Manara amewataka wanayanga kutokua na wasi wasi kwa kukosekana kwa wachezaji hao kwa kuwa kocha anafahamu na kwa ukubwa wa Yanga washajua nini cha kufanya.

Katika barua yake kwa FIFA, klabu ya Yanga imeeleza wazi kusikitishwa na klabu ambazo wachezaji wao walikua wanazichezea na hiyo imefanyika kwa makusudi hivyo haioni haja ya CAF kuwazuia wachezaji hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live