Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaiponeza Simba kwa usajili wa Manzoki

Manzoki Pic Data Manzoki

Sun, 7 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Yanga Simon Patrick amesema usajili wa Cesar Lobi Manzoki ndani ya Simba ni usajili mzuri na wa kiwango cha juu ambapo amemwagia sifa mshambuliaji huyo wa Vipers kuwa atawasaidia watani wao klabu ya Simba.

“Manzoki ni mchezaji mzuri sana na ni kitu ambacho naweza nikawapongeza watani zetu wamepata mchezaji mzuri na tuna Imani atawasaidia namtakia kila lakheri ni mchezaji mzuri tunampenda sana na tunamsapoti akiwa hapa Tanzania.” amesema Simon Patrick

Aidha CEO ameongelea kuhusu tukio la kilele cha wiki ya wananchi ambapo amebainisha kuwa hadi sasa zaidi ya mashabiki 42800 wameshakata tiketi ya kuingia uwanjani huku lengo likiwa ni watu 54000 ambao wanatarajiwa kununua tiketi kwa ajili ya kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya Vipers ya nchini Uganda leo katika mchezo wa kirafiki kuazimisha wiki ya wananchi, mchezo ambao uanatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1 kamili usku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live