Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaipigisha kwata Polisi, Mayele atetema

Screenshot 20221217 215228 Instagram Yanga yaipigisha kwata Polisi, Mayele atetema

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imeendelea kuonesha makali yake kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya leo kufanikiwa kuichapa Polisi Tanzania kwa mabao 3-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza Yanga haikufanikiwa kupachika bao lolote licha ya kupata nafasi nyingi za wazi ambazo hazikuweza kutendewa haki na wachezaji wa Yanga.

Mabao ya Yanga yamefungwa na nyota wao Jesus Moloko, Fiston mayele na bao la tatu lilifungwa na Clement Mzize na kufunga mahesabu ya mabao 3-0 kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na burudani ya kutosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live