Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaipiga mkwara Simba Dabi ya Kariakoo

Ahme Ally Na Kamwe Ally Kamwe na Ahmed Ally

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga wameanza tambo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Siku tano zimebaki kabla ya watani hao wa jadi kumenyana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Mtu wa karibu na benchi la Ufundi la Yanga, amesema kuwa: “Kila mmoja anajua kuhusu mchezo wetu dhidi ya Simba, benchi la ufundi limebainisha kuwa limewaandaa wachezaji kisaikolojia kushinda.

“Baada ya mechi dhidi ya Al Hilal tutaanza kufanya maandalizi, lakini ukweli ni kwamba hatutawaacha salama hao Simba.”

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, aliliambia Spoti Xtra kwamba, mchezo dhidi ya Simba ambao upo mbele yao, wanautambua, hivyo wanajipanga kushinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live