Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaipa mtihani Geita Gold Kirumba

Bakari Nondo X Maxi Nzengeli Yanga yaipa mtihani Geita Gold Kirumba

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Uongozi wa Geita Gold umesema unafikiria kubadilisha uwanja katika mechi zake dhidi ya Yanga kutoka ule wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kwani wamekuwa wakipoteza michezo yao kwa namna ambayo wanaamini siyo kwa ubora uwanjani bali mambo mengine nje ya uwanja.

Timu hiyo ilipoteza kwa mabao 3-0 juzi mbele ya Yanga uwanjani hapo ukiwa ni mchezo wa tatu mfululizo wanapoteza wanapokutana na Yanga huku wakishindwa kufunga bao lolote. Timu hiyo hutumia uwanja huo kwa mechi zake mbili za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wanaohudhuria michezo hiyo, lakini bado wamekuwa hawapati ushindi.

Akizungumza baada ya kichapo hicho, Ofisa Habari na Mawasiliano Geita Gold, Samwel Dida alisema kwamba uongozi unafikiria kuhamisha eneo la mechi zao dhidi ya Wana Jangwani huku akiamini kukamilika kwa uwanja wao wa Magogoni Januari, 2024 wenye uwezo wa kubeba watazamaji zaidi ya 15,000 itakuwa suluhisho.

Alisema uwanja huo umefikia asilimia 85 na tayari wamepatikana wakandarasi wapya kumalizia eneo la kuchezea hivyo wakianza kutumia dimba hilo watakuwa kwenye ubora mkubwa, huku akikiri kuwa kupoteza mchezo wa pili mfululizo kunawanyima usingizi hivyo uongozi unapaswa kukaa chini kutafakari kwa kina shida iko wapi ili warekebishe kwani hawako sehemu salama.

"Kuna namna ambavyo tumekuwa tukipoteza mbele ya Yanga siyo kwamba wanatuzidi sana mbinu tumefikiria pia tuangalie namna ya kubadilisha uwanja labda sisi na Yanga tukikutana Kirumba haitupi matokeo mazuri, kwa hiyo Magogo Stadium ikikamilika tutabadilisha hali hii haimaanishi hatutacheza tena Kirumba.

"Kuna vitu vingi nje ya uwanja ambavyo vinatokea na sisi utawala tumeshaviona tunavifanyia kazi naamini kuna haja ya kumaliza uwanja wetu kwa kasi, naamini ukimalizika Januari, 2024 tutafanya vitu vizuri zaidi ya hivi ambavyo vinaonekana katika viwanja ambavyo hutujavizoea," alisema Dida

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: