Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaikera Simba

Chama Phiri Ll Yanga yaikera Simba

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa imefikia wakati sasa watani zao wa jadi, Yanga wanajiamini kuifunga Simba ama kutoka nayo sare kila wanapokutana.

Ahmed amesema hayo jana Jumapili, Oktoba 23, 2022 mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliowakutanisha Simba na Yanga ambapo timu zote zilitoka sare ya bao 1-1 katika Dimba la Mkapa.

"Imefikia kipindi (Yanga) amekuwa comfortable kwamba kwa huyu (Simba) naenda kuchukua sare au naenda kumfunga, hicho ndicho kitu kinatuumiza sana kichwa sisi kama Simba sports club"

"Afrika hii hakuna timu itapangiwa na Simba halafu ikawa comfortable kwamba naenda kupata sare au naenda kuwafunga (Simba), ni Yanga pekee akipangiwa na Simba anakuwa hana wasiwasi, hicho ndicho kitu kinatuumiza sana," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live