Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaigia kambini kuisoma Namungo

Nembo Kikosi cha Wanajangwani, Yanga SC

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

Klabu ya yanga imesema baada ya kupata ushindi kwenye ligi Kuu katika michezo mitano mfululizo wako kwenye maandalizi ya kwenda kuivaa Namungo katika uwanja wa ilulu mjini Lindi Novemba 20, ili kuendeleza rekodi ya kushinda mechi kwa asilimia 100.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli, amesema kikosi hicho kilichopewa mapumziko ya siku mbili baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting Jumanne iliyopita, kimeingia kambini jana, huku baadhi wakiitwa kwenye vikosi cha vya timu ya taifa.

"Kwanza tunawashukuru sana mashabiki wetu wa Yanga kwa jinsi walivyokuwa wakijitokeza kwenye mechi zetu mbili za nyumbani ili kuwapa morali vijana wetu kupambana zaidi uwanjani. Zimekuwa mechi mbili zenye manufaa sana na tumevuna pointi sita ambazo zimetuwezesha kufikisha pointi 15 mpaka sasa tukiwa kileleni," amesema Bumbuli.

Amesema baada ya mapumziko ya siku mbili, Jumanne na Jumatano, jana kikosi hicho kilitarajia kurejea tena kambini, lakini kikiwakosa baadhi ya nyota ambao watakuwa wanakwenda kutumikia timu za taifa.

Chanzo: ippmedia.com