Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaigeuzia makali Ihefu

0e30d4c359cc058ab96aa2f2cd116789 Yanga yaigeuzia makali Ihefu

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Tanzania Bara, Yanga leo watakuwa ugenini kuikabili Ihefu FC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Yanga ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 40 inaingia katika mchezo huo ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja tangu msimu huu ulipoanza Septemba 6, mwaka huu.

Yanga inakutana na Ihefu ambayo mwenendo wake si mzuri kwani hadi sasa imeshinda michezo mitatu na hivyo kushika nafasi ya tatu kutoka mwisho ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo 16.

Lakini mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na ubora ulioneshwa kwa vikosi vyote katika michezo yao iliyopita.

Yanga imetoka kupata ushindi wa mabao mengi, ikiifunga Mwadui 5-0 na Dodoma Jiji mabao 3-1, hulu Ihefu nayo ni kama gari imewaka sasa kwani walishinda dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 na KMC bao 1-0.

Kocha wa Yanga, Cedric Kaze amesema wamejipanga vyema kwa mchezo huo na malengo yao ni kusaka ushindi kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo na kuziacha timu nyingine kwaa mbali katika msimamo wa ligi.

“Kwa michezo iliyopita wachezaji wamebadilika na kuonesha ushindani kwenye eneo la kufunga sehemu ambayo ilikuwa inaniumiza kichwa, tunajua Ihefu wamejipanga lakini malengo yetu ni kushinda ili kulinda rekodi yetu,” alisema Kaze.

Naye Kocha wa Ihefu, Zuber Katwila alisema wachezaji wake wameanza kujiamini na matarajio yake mchezohuo utakuwa mgumu.

“Siwezi kusema au kuahidi mashabiki ushindi, tumejipanga kutafuta ushindi na tunakwenda kucheza na timu ngumu ambayo haijapoteza mechi lakini mchezo hauwezi kuwa rahisi,” alisema Katwila.

Michezo mingine inatarajiwa kuchezwa leo ni Mtibwa Sugar itakayoialika Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro, wakati JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa KMC Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Chanzo: habarileo.co.tz