Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaifunika Simba

Yanga Pic Data.png Yanga yaifunika Simba

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

SOKA la kisasa ni rekodi kama linavyokuletea Mwanaspoti mechi za watani wa jadi Simba na Yanga, tangu ligi ilipoanzishwa mwaka 1965, utajua nani kavuna pointi nyingi na aliyepata ushindi mnono zaidi.

Simba na Yanga zimewagawanya Watanzania makundi mawili, yanayofanya ubishani uwe mkubwa wakati klabu hizo zinapokutana kwenye majukumu yao.

Katika rekodi hizo zitawasaidia wadau kubishana kwa hoja, kujua timu zao zimefanya nini tangu miaka hiyo mpaka sasa.

MIAKA 55

Huu ni mwaka wa 55, tangu timu hizo zianze kukutana kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, msisimko umekuwa mkubwa, zinapewa heshima ya aina yake, pia zina historia ya kutumika kupigania uhuru, Mwasisi wa taifa la Tanzania, Mwalimu JK Nyerere, alitumia makundi ya mashabiki kutoa elimu namna ya kujiondoa mikononi mwa wakoloni.

Katika miaka 55 ya ushindani baina ya Simba dhidi ya Yanga iliwahi kutokea, Machi 3,1969 Yanga kupewa pointi za mezani na ushindi wa mabao 2-0, baada ya Sunderland ambao kwa sasa ni Simba kugoma kuingia uwanjani.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz