Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaifuata Ihefu Arusha kibabe

Diarra Pacome Job Yanga yaifuata Ihefu Arusha kibabe

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Young Africans SC chenye wachezaji 26, kimesafiri na Ndege ya Shirika la Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kuelekea Arusha kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Ihefu.

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuanzia saa 9 alasiri.

Wachezaji waliosafiri wakiongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ni Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Dickson Job, Kouassi Attohoula Yao, Nickson Kibabage na Lomalisa Mutambala.

Wengine ni Zawadi Mauya, Gift Fred, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’, Jonas Mkude, Farid Mussa, Clement Mzize, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Augustine Okrah, Joseph Guede, Stephane Aziz Ki, Kibwana Shomari, Denis Nkane, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Sheikhan Ibrahim.

Yanga inakwenda Arusha na lengo kuu likiwa ni moja tu kushinda na kutinga fainali kwenda kutetea ubingwa wao.

Ikumbukwe Yanga imetinga nusu fainali baada ya kuichapa Tabora United magoli 3-0 katika hatua ya robo fainali.

Safari yao katika michuano hiyo msimu huu walianzia hatua ya pili ambapo walishinda magoli 5-1 dhidi ya Hausing FC, kisha wakaichapa Polisi Tanzania 5-0. Baadaye wakashinda 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC kabla ya kuiondosha Tabora United kwa magoli 3-0.

Katika mechi hizo nne wamefunga magoli 15 na kuruhusu moja pekee, huku mshambuliaji wao, Clement Mzize akiwa kinara wa ufungaji akifunga magoli matano huku akiwa na hat trick moja mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: