Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaifuata Ahly na hesabu hizi..!Rais atoa neno

Yanga Lomalisa Okrah Maxi Yanga yaifuata Ahly na hesabu hizi..!Rais atoa neno

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimeondoka nchini jana jioni kikiacha staa mmoja huku mabosi wao wakitanganza hesabu zao mpya mbele ya Al Ahly.

Yanga itakutana na Al Ahly kwenye mchezo wa kukamilisha makundi utakaopigwa Machi 2, jijini Cairo, Misri huku timu zote zikiwa zimeshakata tiketi ya kucheza robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rais wa Yanga injinia, Hersi Said amesema kikosi chao kinakwenda kucheza mchezo wa mwisho kikiwa tayari na tiketi ya kucheza robo fainali na wanaenda kutafuta nafasi ya kumaliza kinara wa kundi lao D.

Hersi amesema hiyo itawasaidia kupata wepesi kwenye droo ya kucheza robo fainali na itapangwa na mshindi wa pili wa moja ya makundi yaliyosalia na kuanzia ugenini.

"Sote tunafahamu ukiongoza kundi itakapokuja droo utapata faida nyingi kwanza ni kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani lakini sio hiyo tu utapata nafasi ya kucheza na timu za pili kwenye makundi mengine," amesema Hersi

"Tuna imani kubwa na timu yetu baada ya kuona kiwango chao kwenye mechi tano zilizopita, tunaamini kwa maelekezo ya makocha wetu tunaweza kwenda kupata matokeo mazuri ugenini ingawa utakuwa ni mchezo mgumu.

"Tunawapongeza sana wachezaji wetu na benchi la ufundi kwa juhudi ambazo wamezifanya kwenye mechi hizi, lakini bado tunaona kuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri zaidi huko mbele."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: