Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaiduwaza Ihefu, fainali sasa ni Wananchi na Azam tena

Yanga Aziz WA0007 Wachezaji wa Yanga wakishangilia

Sun, 19 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya fainali kombe la shirikisho la CRDB Bank baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu FC.

Licha ya mchezo kuwa mgumu kwa pande zote mpaka dakika 90 zinamalizika bila nyavu za upande wowote kutikiswa, Wananchi walisubiri takribani dakika 101 kupata bao kupitia kwa Stephane Aziz Ki akipokea pasi safi kutoka kwa Pacome Zouzoua.

Dakika 90 za mchezo huo ambazo zilimalizika kwa matokeo ya 0-0, zilikuwa na ushindani mkubwa, lakini mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi yalibadili hali ya mchezo.

Kipindi cha kwanza dakika ya 40, beki wetu Nickson Kibabage alitolewa uwanjani baada ya kuanguka, nafasi yake ikachukuliwa na Lomalisa Mutambala.

Dakika ya 60, Clement Mzize na Maxi Nzengeli walitolewa nafasi zao wakaingia Pacome na Joseph Guede ambapo kuanzia hapo mchezo ulibadilika na kupelekea ushindi huo uliopatikana ndani ya dakika 30 za nyongeza.

Baada ya ushindi huo, wanakwenda kucheza fainali dhidi ya Azam Juni 2, mwaka huu huku wakiwa na rekodi bora dhidi yao.

Tangu msimu wa 2015-2016, wamekutana na Azam mara mbili kwenye fainali ya michuano hiyo na zote Yanga wameshinda.

Msimu wa 2015-2016 Yanga walishinda magoli 3-1 kisha msimu uliopita 2022-2023 tukashinda tena goli 1-0.

Fainali ya tano kwa ‘Wananchi’ na ya nne mfululizo. Pia itakuwa ni fainali yao ya tatu kukutana na Azam FC.

AET: Ihefu 0-1 Yanga

Tukutane Juni 02, 2024 katika Uwanja wa Babati Manyara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live