Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaichimba mkwara Azam FC

Bumbuli Vs Azam Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Oktoba 30, wakubwa wawili kunako Ligi Kuu ya NBC, wanakutana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Ni Yanga dhidi ya Azam FC, katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, huku kila timu ikiwa imetoka kuvuna alama tatu katika michezo yao ya mwisho, ambapo Yanga wametoka kupata ushindi mbele ya KMC, wakati Azam wametoka kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Namungo.

Sasa Mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga, Hassan Bumbuli amesepata wasaa wa kuzungumza kuelekea mchezo huo wa Oktoba 30.

"Timu tayari imekwisharejea Dar, na wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili ambapo siku moja tumeitumia kumfariji mwenzetu aliefiwa na mzazi wake, Paul Godfrey, kwa hiyo tarehe 22, kikosi kitarejea kambini kwa ajili ya maandalizi dhidi ya Azam"

"Tunautazama kama mchezo mgumu kwa kuwa hivi sasa kila timu ikishajua inacheza na Yanga inafungua maturbo, kwa ajili ya Yanga. Lakini sisi kama Klabu tunajua, walimu wetu wanajua hivyo tunawaambia Azam wajiandae kwa sababu hatuna uwanja mgumu wala mwepesi, hatuna uwanja mzuri wala mbaya zitakuwa zinaguswa na zinafika" ametanabaisha Bumbuli

"Na kama ambavyo tumewaambia tangu juzi kama kuna mtu wanataka kumfukuza basi wamfukuze mapema ili isije kuonekana Yanga ndio sababu ya kumfukuza huyo mtu" amesema Bumbuli.

Azam FC kwa sasa wako kule Cairo nchini Misri, wakijiandaa kuwavaa Pyramids FC katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga kwa sasa ndio kinara katika msimamo wa Ligi akiwa amejikusanyia alama 9 akiwa ameshacheza michezo mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live