Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaichapa Singida FG, yaitumia salam Simba

Yanga 9073 Yanga yaichapa Singida Fountain Gate

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC wameishushia kipigo kizito timu ya Singida Fountain Gate baada ya kuifunga bao 3-0 katika mchezo wa ligi uliopigwa jioni ya leo katika Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Joseph Guede ambaye amefunga mabao mawili dakika ya 42 n 68 huku bao jingine likifungwa na Stephanie Aziz Ki dakika ya 66.

Yanga sasa wanafikisha alama 55 wakiwa kinara kwenye msimamo wa ligi huku wakiwaacha mbali kwa alama 9 watani zao Simba SC wenye alama 46 katika nafasi ya tatu na Azam nafasi ya pili wakiwa na alama 47.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki ameendelea kujikita kwenye kilele cha wafungaji bora akiwa jumla mabao 14 mbele ya Fei Toto wa Azam FC mwenye mabao 13.

Jumamosi ijayo Aprili 20, katika Dimba la Mkapa kutakuwa na kazi ngumu ambapo Simba na Yanga watakipiga huku Yanga wakionekana kuwa bora zaidi kuliko watani zao Simba ambao walitoa kwenye michezo minne ya mwisho hawajapata matokeo, lakini mechi ya dabi haina mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live