Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaichapa Namungo, TFF yatoa msimamo

Yangaz Pic Data Yanga yaichapa Namungo, TFF yatoa msimamo

Sat, 13 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this Author RASMI leo pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa Vijana wasiozidi umri wa miaka 20 limefunguliwa kwa michezo minne kupigwa kwenye viwanja tofauti na matokeo kupatikana huku Yanga, Azam, Tanzania Prisons na Coastal Union wakitakakata.

Mechi za mapema zilizoanza mchana zilikuwa kati ya Ruvu Shooting na Azam ambapo vijana wa Azam wameibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee likiwekwa nyavuni na Paschal Msindo dakika ya 31 kwa shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Ruvu, Mussa Kibwana.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Prisons na  Mtibwa Sugar ambapo maafande hao wameibuka na ushindi wa bao 2-1 na  mabao hayo yakiwekwa kambani na Kelvin Kristoms dakika ya 46 na Josephat Frank dakika ya 74 huku lile la kufutia machozi kwa Mtibwa wakilipata kupitia kwa beki wa Prison Kaburu Mazanda aliyejifunga dakika ya 16 pia Kagera Sugar wameifunga Dodoma Jiji bao 2-1.

Mechi nyingine zingine zilichezwa saa 10:00 jioni ambapo Yanga wamecheza na Namungo na kushinda kwa bao 2-0, huku kule mkwakwani Tanga wenyeji Coastal Union wakiibuka na ushindi wa 2-1 mbele ya Polisi Tanzania, matokeo hayo pia yamefanana na yale ya mchezo kati ya Mwadui na Gwambina ambapo Mwadui wameshinda 2-1.

Katika uzinduzi wa michuano hiyo leo, Mwenyekiti wa soka la vijana taifa kutoka TFF Kharid Abdallah amewasihi wachezaji wa timu zote 18 zinazoshiriki ligi hiyo kuimarisha nidhamu kwani ndio siri kubwa ya mafanikio.

"Kwetu TFF tunazingatia sana nidhamu na tutahakikisha tunaisimamia vyema katika michuano hii, wachezaji wasio na nidhamu watashindwa kuzisaidia timu zao kutokana na adhabu mbalimbali watakazokutana nazo," amesema Abdallah.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz