Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaichapa Ihefu kwa Mkapa, Mayele atupia bao la 15

K Musonda Mshambuaji wa Yanga, Kennedy Musonda akiwatoka walinzi wa Ihefu

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga wamelipa kisasi kwa Ihefu FC ambao walivuruga rekodi yao ya kutopoteza mchezo Novemba 29, 2022.

Mchezo huo ambao Yanga walipoteza kwa magoli 2-1 ulihitimisha safari yao ya michezo 49 ya Ligi pasipo kupoteza sasa leo katika Uwanja wa Mkapa Yanga wamelipa kisasi.

Bao pekee la Fiston Mayele akiunganisha pasi ya kichwa ya Jesus Moloko lilitosha kuwahakikishia wananchi alama tatu na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Yanga ambao imewakosa baadhi ya nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza kama Khalid Aucho, Aziz Ki, Bernard Morisson, Yanick Bangala imeondoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Ushindi huo unawafanya Yanga kufikisha alama 53 baada ya michezo 20 ya Ligi huku Simba wakiwa na alama 44 baada ya michezo 19 ya Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live