Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaichapa Green Warriors 4-0

Musonda Duke Yanga yaichapa Green Warriors 4-0

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jioni ya leo, kikosi cha timu ya Young Africans SC, kimecheza mechi ya kirafiki kujiweka sawa kuelekea mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O.

Mchezo huo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wetu wa mazoezi uliopo Avic Town, Kigamboni, Young Africans imeibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Green Warriors.

Wafungaji wa magoli hayo ambayo yote yamefungwa kipindi cha kwanza ni Kennedy Musonda, Clatous Chama, Jean Baleke na Duke Abuya.

Yanga kucheza mechi hiyo ya kirafiki ni sehemu ya kukiweka sawa kikosi kilichotoka kushinda Ngao ya Jamii, huku pia Jumamosi ijayo ya Agosti 17, 2024 wakiwa na mechi dhidi ya Vital’O ya Burundi katika mchezo wa kwanza hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya mchezo huo wa kwanza, Yanga watarudiana Agosti 24, 2024 huku yote ikichezwa Dar es Salaam kutokana na wapinzani wao kuuchagua Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zao za nyumbani baada ya kukosa viwanja vyenye hadhi ya kimataifa nchini kwao Burundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: