Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaibamiza CR Belouizdad bao 4G na kutinga robo fainali CAFCL

Yanga 4 WA0024 Yanga yaibamiza CR Belouizdad bao 4G na kutinga robo fainali CAFCL

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga ya Dar es Salaam, imetinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria mchezo wa Kundi D Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 8 ikishika nafasi ya pili nyuma ya Al Ahly inayoongoza kundi ikiwa na pointi 9, hata kama Yanga itapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Al Ahly wiki ijayo mjini Cairo, Misri, kisha CR Belouizdad yenye pointi tano ikishinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mediama na kufikisha pointi nane, bado itakuwa imefuzu robo fainali.

Hatua hiyo inatokana na kanuni za mashindano hayo yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), ambapo ikitokea timu zikalingana pointi, basi hatua ya kwanza ni kuangalia mchezo baina yao nani alishinda. Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliofanyika Algeria, Yanga ilifungwa mabao 3-0, hivyo kwa ushindi wa leo wa mabao 4-0 Yanga ipo juu.

Wananchi wanaandika historia ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria kwenye hatua ya makundi.

FT: Young Africans 4-0 CR Belouizdad

⚽️ Mudathir Yahya 43'

⚽️ Aziz Ki 46'

⚽️ Kennedy Musonda 48'

⚽ Joseph Guede 84'

MSIMAMO KUNDI D

1. Al Ahly ——— 9

2. Yanga Sc ——— 8

3. CR Belouizdad ———5

4. Medeama ———4

Yanga SC imefuzu moja kwa moja kwa kuwa mbabe wa 'head to head' kati yake na CR Belouizdad, kwa maana hata kama Belouizdad atashinda mechi ya mwisho hawezi kufuzu.

Itakumbukwa mechi ya kwanza Yanga ilipoteza 3-0 kabla ya kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live