Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yagoma kupigiwa ramli

Yanga Tano Pacome Maxi 191929 Yanga yagoma kupigiwa ramli

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaandika Alikamwe; Mwezi huu tuna mechi 5. Mechi 4 za ligi kuu na moja ni robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Alhamdulillah. Mpaka sasa tumeshapata pointi 6 kati ya 12 tunazoitafuta kwenye mechi za Ligi Kuu ndani ya mwezi huu. Bado pointi 6 nyingine zimebaki.

Niwaombe wananchi. Muda wa huu wachambuzi na makolo wakichambua na kupiga ramli zao kwenye mechi yetu ya robo fainali. Sisi focus yetu kwanza iwe kwenye pointi 6 za Ligi Kuu.

Hizi mechi 2 zinazofata [vs Geita Gold na Azam FC], zinaweza kuwa na taswira nzuri ya kutetea uchampion wetu wa ligi. Hivyo ni lazima tuziendee hizi mechi kikubwa mno.

Huu upele wa Mamelodi unaowawasha watu hivi sasa, sisi ndio wakunaji. Tutulie muda wake ufike na ndio wataijua vizuri yanga afrika inafananaje.

Naomba kesho In Shaa Allah wananchi tukutane azam complex, kuzisaka pointi 3 dhidi ya Geita. We are Young Africans Sports Club.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: