Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yafunguka kutoaanika pesa waliyomuuza Fei Toto

Feisal Azam Hsg Yanga yafunguka kutoaanika pesa waliyomuuza Fei Toto

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema maamuzi ya kumuuza mchezaji wao Feisal Salum kwenda Azam FC yametokana na timu hiyo kupokea ofa yao ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo.

Kamwe amesema hayo baada ya Yanga kumalizana na mchezaji huyo kisha kumuuza kunako klabu ya Azam kwa mkataba wa miaka miwili.

Aidha, kuhusu thamani ya mchezaji huyo alivyo uzwa kwenda Azam FC, Kamwe amesema itabakia kua Siri kulingana na makubaliano kati ya timu hizo mbili na mchezaji.

Itakumbukwa kwamba usiku wa Juni 5, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan aliuomba uongozi wa Yanga kumalizana na suala la mchezaji Feisal Salum Ili aendelee kucheza.

"Baada ya kamati iliyokuwa ikishughulikia sakata la mchezaji Feisal Salum kutoa maamuzi yake, Klabu ya Yanga tulitoa taarifa yetu kuhusu sakata lile, tulitoa options tatu au nne ya nini kifanyike.

"Kwanza Feisal aripoti kambini, pili tuko tayari kuvoresha maslahi ya mkataba wake na namba tatu klabu ambayo inamtaka ifuate taratibu za usajili ilete ofa Yanga.

"Katika hayo manne limefanyika moja la Azam FC kuwa waungwana na kuja kugongana hodi kuulizia bei ya Fei Toto ili waweze kumnunua.

"Maamuzi ya Yanga kumuuza Fei Toto yanatokana na maslahi mapana ya soka, asitokee mtu akaingiza dhana nyingine na hii tulisema tangu kamati ilipotoa maamuzi, tunashukuru Azam wamefuata taratibu na dili tumemaliza kufanya biashara na tumelimaliza.

"Tunamtakia Fei Toto kila la kheri akaendeleze makombora yake kwenye mazingira yake mapya ya kazi na Mwenyezi Mungu amjalie mafanikio mema.

"Kuhusu dau la Yanga kumuuza Fei Toto, ni dau ambalo kwa makubaliano ya pande zote mbili halitawekwa hadharani. Hivi sio vitu vigeni kwenye soka, hata nje haya mambo yanafanyika sana," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: