Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yafunga kambi, mastaa ruksa kula bata

Yangasc Kosi Yanga yafunga kambi, mastaa ruksa kula bata

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habri na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe amezungumzia mipango ya timu yake katika wakati huu mapumziko na malengo yao kwa wachezaji waliong’ara na timu hiyo msimu huu.

Kamwe amesema kuwa kwa sasa Kambi ya timu imevunjwa na kuwaruhusu wachezaji kwenda mapumziko kabla ya kurejea tena hapo baadaye kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ujao.

“Tayari kambi yetu ya Yanga imeshavunjwa, wachezaji ambao wanakwenda kwenye majukumu ya timu zao za Taifa wamesharipoti. Baadhi wamesafiri kutokea Zanzibar na wale ambao hawajaitwa tumewapa mapumziko, kitaalam kwa sasa tupo kwenye off-season ambacho ni kama holiday.

“Ni mapema sana kwa sasa kuzungumzia kambi yetu ya msimu ujao, akini kwa sasa tunaendelea na sherehe. Ndiyo kipindi cha Wanayanga kuvimba, kutamba na kujivunia klabu yao.

“Tarehe 9, mwezi huu wa Juni tutakuwa na mkutano mkuu wa klabu, niwaambie viongozi wa matawi kwamba matawi yao yanakidhi kama katiba inavyotaka ili wanachama wao waweze kuhudhuria mkutano huu,” amesema Kamwe.

Rais wa Yanga SC Injinia Hersi Said amesema kuwa kuanzia leo June 05, 2024 wamewapa mapumziko wachezaji wao ya mwezi moja na wataaanza kurejea kuanzia mwezi Julai kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano ya 2024 - 2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live