Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yafanya maamuzi magumu kwa Bangala na Djuma

Yanga Djuma Bangala 50 Yanga yafanya maamuzi magumu kwa Bangala na Djuma

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umesema kuwa utatoa taarifa rasmi kuhusu maamuzi yaliyofikiwa baina yao na wachezaji wao wa Kimataifa, yanick Bangala, Djuma Shabani, Mamadou Doumbia na Fiston Mayele.

Hayo yamesemwa na ofisa Habari wa Kalbu ya yanga, Ali Kamwe wakati akihojiwa kuhusu kutokuonekana kwa wachezaji hao kwenye tamasha la Siku ya Mwananchi juzi huku wakitajwa kuwa tayari wameshaachana na kikosi cha timu hiyo.

“Ni kweli hawakuonekana hawa wachezaji wakimataifa ambao tulikuwa nao msimu uliopita na niwaambie mashabiki na wananchama wa yanga kwamba tumepokea maswaIi mengi kutoka kwao na klabu itakwenda kutoa taarifa rasmi inayoeleza taarifa za hawa wachezaji hao na maamuzi ya klabu ambayo tumeyafikia kwa hawa wachezaji.

“Sio hawa tu, hata Mamadou Doumbia pia watu wamemuulizia, tutatoa taarifa kuhusu nini ambacho uongozi umekiamua kwa wachezaji hawa.

“Kinachonishangaza mnaweka ajenda tuzungumze ambao hawakuja tusizungumze waliokuja, sio tuulize waliopo na performance zao zikoje,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: