Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yafanya jambo zito Afrika Kusini

Yanga 17290 Yanga yafanya jambo zito Afrika Kusini

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya Yanga imeendelea kutanua wigo kwa kuongeza matawi ya mashabiki zake kimataifa baada ya kufungua tawi jipya nchini Afrika Kusini.

Yanga wapo Sauzi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa kesho Ijumaa, hivyo wametumia fursa hiyo kufungua tawi na kutanua wigo wao wa fans engagement.

"Klabu ya Young Africans SC inaendelea kuweka rekodi ya kuzindua matawi nje ya mipaka ya Tanzania. Tumefungua tawi kule nchini DR Congo, na leo tumezindua tawi lingine hapa nchini Afrika Kusini. Tunaposema sisi ni wakubwa tunamaanisha," Ibrahim Samwel - Mkurugenzi wa Masoko, Wanachama na Mashabiki Young Africans SC.

WANANCHI WAPO HADI MAREKANI

"Niweke rekodi sawa, sisi tuna matawi lukuki nje ya mipaka ya Tanzania. Kwa Mfano kule Marekani tunalo tawi la uanachama," amesema Eng. Herse Said Rais wa Yanga SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live